DUPSA REPORTS


DODOMA UNIVERSITY PROJECT PLANNERS’ STUDENTS ASSOCIATION
(DUPSA)
TAARIFA YA UTENDAJI WA DUPSA (26 MEI 2010/16 APRIL 2011).
Mheshimiwa mwenyekiti,
Mheshimiwa M/Mwenyekiti,
Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu,
Mheshimiwa Mtunza Fedha,
Waheshimiwa Maafisa wetu wa habari,
Waheshimiwa wajumbe wa kamati kuu,
Waheshimiwa wageni waalikwa,
Waheshimiwa Wanachama,
Ndugu zangu Msiokuwa wanachama,
Mabibi na Mabwana,
Habari za saa hizi…………………………….

Ndugu wajumbe niruhusu nianze kwa kutoasalamu za pole kwa wote waliopatwa na matatizo katika mwaka huu wa kiuongozi ndani ya DUPSA.Kuugua,kuuguliwa na hatakuondokewa na wapendwa wetu ni baadhi ya matukio yaliyojitokeza.Mungu awapumzishe Mahali stahiki.Amen.
Ndugu wajumbe,  ni siku ya 26 ya Mwezi wa tano,2010;uongozi unaoelekea kumaliza muda wake hivi  punde  ulipokabidhiwa uongozi kutoka katika mikono ya Uongozi wa mpito,uliokuwa unashikilia uongozi tangu kuanzishwa kwake rasmi na kusajiliwa katika ofisi ya mwadili wa wanachuo,chuo kikuu cha Dodoma; mnamo tarehe 26 September,2009.
Kama jumuiya DUPSA;ina dira  na malengo yake.Ni  katika dira na malengo hayohayo Uongozi umekuwa ukitenda  na kutekeleza majukumu yake.Ni katika mengi  uongozi na wanachama wote tumeweza kufanikiwa.Hata hivyo zimekuwepo changamoto kadhaa ambazo ni pamoja na matatizo ya kimazingira,hulka ya mihula ya masomo,hali ya kiuchumi na ukiritimba katika taasisi mbalimbali zulizozishirikisha  katika juhudi za kuifikisha  katika kilele cha mafanikio.
Ndugu wajumbe niruhusu sasa nifafanue sehemu ya mafanikio na changamoto tulizokutana nazo.
Mafanikio
Kwanza, Tumefanikiwa sana koungeza idadi ya wanachama kutoka 65 waliokuwepo wakati tunakabidhiwa uongozi hadi 152 hivi sasa tunapoondoka katika uongozi.
Pili,tuweza kuendesha Semina na warsha kadhaa kama ifuatavyo:
  1. 07 Mei,2010:warsha iliyobeba kichwa “The mechanisms on the Preparation and Application of Medium Term Expenditure Framework(MTEF);wawezeshaji wan je.
  2. 05 Juni,2010: warsha ikibeba kichwa: Labor Market and labor Market Reforms in Tanzania;wawezeshaji wa n je.
  3. 26 Machi,2011: Semina chini ya kichwa:The system for procurement of common use items and services(CUIS) Through agreement framework.Kubwa zaidi wawezeshaji walitoka Miongoni mwetu,jambo ambalo tafsiri yake sahihi ni kuwa Tumefanikiwa kujenga uwezo wa ndani wa kuendesha warsha na semina kama ilivyoainishwa katika malengo yake.
  4. 2 April,2011:Warsha ikibeba kichwa Development Programme planning and Management,iliyofanyika nje ya mazingira ya chuo kwa mara ya kwanza huku wakishuhudiwa wawezeshaji kutoka nje.
Tatu,tumeweza kuongeza mapato ya chama kwa 67.75%,kama ilivyoainishwa katika taarifa ya fedha ya mweka hazina.
Changamoto
Ndugu wajumbe,Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto kadhaa ambazo tumekumbana nazo wakati wa kutekeleza majukumu ya uongozi:
                                i.            Mwitikio mdogo wa wanachama katika vikao,na hivyo kupunguza ufanisi wa kiutendaji kwan kukosekana kwao kumetunyima mawazo mazuri,kuhoji,mapendekezo,ushauri na p engine maonyo pale ilipobidi kwa maslahi ya jumuia.
                              ii.            Madeni:wanachama wamekuwa wanasuasua katika ulipaji ada ya uanachama na hivyo kuinyima Jumuia mapato halali kwa ajili ya shughuli mbalimbali za chama.Mfano mpaka leo pesa iliyopo mikononi mwa wanachamani( madeni )ni  shilingi 758,000/-
                            iii.            Shughuli za kitaaluma na matukio yasiyokuwa katika mpangilio wa kawaida wa kalenda ya chuo.mfano:migomo ya wanachuo .Hii imeathiri sana mipango na malengo  ya DUPSA kwani ilipelekea baadhi ya shughuli za jumuiaya kuahirishwa.
                             iv.            Kipato kidogo cha jumuia,jambo ambalo limeathiri maandalizi  ya matukio mbalimbali ya Jumuiya.Mfano uwezo mdogo wa kuwaleta wawezeshaji wa kulipwa.hii imepunguza ufanisi wa Ki-jumuiya.
Udhaifu na Mapungufu:
Ndugu wajumbe wa mkutano mkuu,kiongozi mzuri ni Yule ambaye anatimiza majukumu yake,lakini pia akaweza kutambua changamoto zilizopo na pia kutambua udhaifu na mapungufu yaliyojitokeza katika kipindi cha uongozi wake: Sisi pia ni viongozi wa aina hiyo:
Kwanza,mfumo usiokuwa  rasmi wa utoaji taarifa hasa fedha,jambo ambalo lingeweza kuibua mashaka na minong’ono isiyokuwa ya lazima juu ya usalama wa fedha zao.
Pili,kutokuzingatia na kusimamia baadhi ya vipengele vya katiba haswa kile cha kufuatilianwanaodaiwa na kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu.
Tatu, mfumo usiokuwa rasmi wa kuhamasisha wanachuo  ili kujiongezea wanachama wapya umekuwa haudhihiriki.Hivyo kuifanya jumuiya kukosa fursa hiyo ya kujiongezea uigo kakita tafsiri hiyo.
Nne,kucheleweshwa kwa vitambulisho vya uanachama mara tu wanachama wapya wanapojiunga na DUPSA.
Ndugu wajumbe, pamoja na changamoto na matatizo hayo yaliyojitokeza, ni dhahili kuwa viongozi wetu wamefanya kazi kubwa nay a kutukuka sana.Hivyo kwa niaba ya Jumuiya ya DUPSA nitoe shukrani zangu za dhati kwa Viongozi wote kama ifuatavyo
Kwanza,Mwenyekiti na Ofisi yake yote;kwa kujituma  na kusimamia shughuli zote za jumuiya bila kuchoka.Moyo wa kujitolea ulionekana muda wote wa viongozi hawa.tunawashukuru sana na kuwaomba mviendeleze vipawa hivyo mlivyojaliwa na Mungu.Mwenyekiti hongera sana.jumuiya inautambua mchango wako.
Pili,ofisi ya Katibu.Tunashukuru sana,nyaraka zi salama.Nimshukuru kwa namna ya pekee naibu wangu.ujio wake katika ofisi yangu ulikuwa neema.Yamkini bila yeye mambo yasingekuwa murua kama tunavyoyaona.Ahsante sana na nikutakie mafanikio katika uchaguzi ujao.ufanikiwe wajumbe wakukubali si kwa kukufahamu kwa jina tu, bali kutokana na kazi yako mahiri.
Tatu,Mtunza fedha,pole sana kwa changamoto za mahesabu. na kutokuwa na taaluma ya fedha,umeweza kuimudu  nafasi hii kwa ustadi mkubwa.Fedha zetu zi salama kabisa.hongereni sana na Mungu akujazi uendelee kuwa na moyo wa uaminifu  na wa kutumika.
Nne, niwashukuru maafisa habari,pamoja na changamoto nyingi zilizoikabili ofisi yao,tumeweza kufanya kazi hadi siku ya leo tunapoikabidhi ofisi.
Nitakuwa Mchoyo wa fadhila,taarifa hii isipotambua mchango mkubwa wa wajumbe wawakilishi katika kamati tendaji.Ndugu wanaDupsa, hakika mlikuwa na uwakilishi uliotukuka.Walitubana kweli ili kuhakikisha maslahi ya jumuiya yanalindwa.Renatha Sindabaha, Azizi Mhanda, Zaituni Msongo na Magesa Lameck.Nyinyi ni mashujaa.Furaha yangu kwenu inazidi pale ninapoona nusu yenu inagombea nafasi za Uongozi.Ni imani yangu wanajumuiya watawapa nafasi muwatumikie kwani uwezo mnao.

Wito,Maoni na Mapendekezo
Uongozi ni kama mbio za kijiti ambapo mkimbiaji mmoja hukimbia na kulazimika kumkabidhi kijiti mkimbiaji mwingine ili aendelee na mbio, na hatimaye kuibuka na Ushindi ambao huwa ni tunu kwa wote wawili.Tukiguswa na hilo, tunatoa wito,maoni na mapendekezo yafuatayo:
Kwa wale watakaopitishwa,Tambueni kuwa cheo ni dhamana.umeaminiwa nawe jiaminishe.Tumika vilivyo.
Aidha jueni kuwa DUPSA haina mshahara.Ni kazi ngumu ya kujitolea ambayo msingi wake mkuu ni kujituma,kuwajibika na p engine  lugha kali nay a matusi.Wewe kama kiongozi mzuri yafyonze yote na kuyafanyia kazi.Usibishane ili uweze kujitofautisha kwa urahisi.Maana wenzetu husema”NEVER ARGUE WITH THE FOOL,PEOPLE MIGHT NOT NOTICE THE DIFFERENCE”
Kuhusu katiba natoa wito ipitiwe tena na kufanyiwa marekebisho ili kuendana na mahitaji ya sasa.
Aidha ziandaliwe kanuni ndogondogo ambazo zitasaidia kuweka msingi wa kiuongozi katika mambo madogomadogo yasiyokuwa ya kikatiba.
Uanzishwe utaratibu wa utoaji taarifa ya mapato na matumizi kwa muda mfupi utakaowekwa na wanajumuiya.
Aidha Ofisi ya Mwenyekiti ipewe muhuri wake ili kutenganisha ngazi za kimaamuzi ndani ya Jumuiya,badala ya ofisi hiyo kushirikiana muhuri na ofisi ya katibu.
Mkutano mkuu ufanyike siku tofauti na ya uchaguzi ili kutoa mwanya wa kutosha kwa wanachama kuhoji na kujadili mambo mengi zaidi kuliko ilivyo sasa.
Wanadupsa,DUPSA, imekua sasa, hivyo ni imani yetu kuwa uongozi ujao utafikiria zaidi kufanya kazi nje ya chuo.Tunaamini sasa uwepo wa safari za mafunzo(study tours) umefika wakati wake….si wakati tena wa kufanya kazi za ndani tu.Ebu twende nje sasa.
Jina la DUPSA limekomaa,hii itarahisisha zoezi la kupata wafadhiri na wadhamini wa shughuli hizo.
Haya yote yatawezekana iwapo tutachagua viongozi makini na bora.Tuache  ushabiki.Zipo dalili zinazoonesha mtazamo wa kisiasa kunyemelea akili na ufahamu na hivyo kuleta upako wa kisiasa,katika harakati za kutafuta uongozi.Nawaonya watu hawa na kuwaeleza kuwa hapa si mahali pao.Watafute mlango wa kutokea na wawaache wanataaluma waiendeleze DUPSA  kitaaluma na wala si kisiasa.
Na hapa ieleweke wazi kuwa wanachama ni nyinyi wenye mamlaka ya mwisho ya kufanya maamuzi.Tumieni\
 mamlaka hiyo ya kikatiba kumwajibissha kiongozi yeyoye anayeelekea kuiharibu jumuiya.
Mwisho,nitoe wito kwa kina dada.mnaweza. ebu jitokezeni katika nafasi mbalimbali za uongozi.Mwitikio wenu katika shughuli za Jumuiya bado ni mdogo.Ni imani yangu wale waliojitokeza katika nafasi za uongozi wanachama watawaamini na kuwapa nafasi.naamini hamtawaangusha,nao hawatawaangusha watawapa nafasi.Hivyo msiangushane
Niwashukuruni nyote Kwa ushirikiano mliotoa kwa uongozi unaomaliza muda wake,na kuwatakia kila lililo la heri,Baraka na fanaka katika kuiimarisha DUPSA
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
………………………………………………….
Mulisa Charles
Secretary general